Wazazi wamekusanyika katika shule hiyo kujulia hali ya watoto waoImage caption: Wazazi wamekusanyika katika shule hiyo kujulia hali ya watoto wao
Mamia ya wavulana hawajulikani waliko baada ya watu waliyojihami kwa silaha kuwateka kutoka shule moja ya bweni kaskazini mwa Nigeria usiku wa Ijumaa.
Wazazi waliojawa na wasisi wasi wamekusanyika katika shule hiyo kusubira taarifa kuhusu watoto wao huku vikosi vya usalama vikiendelea kuwatafuta katika msitu ulioko viungani mwa mji wa Kankara
Karibu wanafunzi 800 wanasomea shule hiyo ya bweni ya wavulana pekee.
Makundi yaliyojihami mara kwa mara yanawateka watu na kisha kudai kikombozi katika eneo la kaskazini -magaribi mwa Nigeria. Kufikia sasa watu hao hawajatoa masharti yoyote.
Awali msemaji wa Rais wa Nigeria, Garba Shehu, amesema anaamini ni watoto 10 waliotekwa na kwamba wengi ni wale ambao wametoroka.

No comments:
Post a Comment