Search This Blog

Thursday, December 24, 2020

Makaburi mengine ya umati yapatikana Libya


Afisa wa mawasiliano wa Taasisi ya Utafutaji na Utambuzi wa Serikali ya Libya Abdulaziz Jaferi, alizungumza na wanahabari na kuarifu kugunduliwa kwa makaburi mengine mawili ya umati katika eneo la Rabit mjini Terhune.

Jaferi, ambaye hakutoa maelezo juu ya shughuli inayoendelea katika eneo la makaburi, alibaini kuwa uchunguzi uliofanywa katika mji huo chini ya usimamizi wa timu maalum bado unaendelea.

Kama sehemu ya operesheni ya "Dhoruba ya Amani" iliyozinduliwa mnamo Machi 25, jeshi la Libya lilianzisha shughuli ya udhibiti wa mipaka yote ya kiutawala ya mji mkuu wa Tripoli tarehe 3 Juni na mji wa Terhune tarehe 5 Juni .

Baada ya kukombolewa kwa mji wa Terhune, ambao wanamgambo wa Haftar waliutumia kama kituo cha operesheni na maandalizi ya mashambulizi yao ya miezi 14 Tripoli, mamlaka ya Libya ilifikia makaburi mengi na maiti nyingi kwenye maeneo ya karibu.

Katika taarifa iliyotolewa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa mnamo tarehe 22 Juni, ilibainika kuwa taarifa za kuaminika juu ya makaburi hayo ziliwasilishwa kwa Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu.

Wanamgambo wanaomuunga mkono Haftar "Kaniyat" wanatuhumiwa kwa mauaji ya kiholela ya raia na makabila wanayoona kama wapinzani katika mji wakati walipokuwa wakidhibiti Terhune.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...