Search This Blog

Saturday, December 19, 2020

Kambi za JKT Nachingwea na Makotopora zafanya kweli kuinua uzalishaji wa korosho

Kambi za Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) za Nachingwea na Makotopora katika kuhakikisha uzalishaji wa zao la Korosho nchini unaongezeka, zimeanza kuzalisha miche bora ya mikorosho.

Akizungumza na Muungwana Blog mjini Nachingwea,mkuu wa kikosi namba 843( 843 KJ) kilichopo wilayani Nachingwea mkoani Lindi, Luteni Kanali Nyagalu Malecela alisema vikosi hivyo viwili katika kuadhimisha miaka 59 ya Uhuru wa Tanzania bàra(Tanganyika) viliamua kuendelea kutoa elimu kwa vitendo kwa wakulima nchini ili wazijue njia nzuri za uzalishaji miche ya mikorosho.

Kamanda Malecela alisema zoezi lilianza kanda ya Kusini katika mikoa ya Lindi na Mtwara. Ambapo sasa limehamia kanda ya Kati. Nakubainisha kwamba tayari miche 300,000 imezalishwa katika kitalu cha Mkiwa kilichopo mkoani Singida.

Kamanda huyo wa 843 KJ alisema kuanzi tarehe 25.12.2020 miche hiyo ya mikorosho ya muda mfupi ambayo mbegu zake zimezalishwa katika taasisi ya utafiti wa mazao ya kilimo kittuo cha Naliendele( TARI- Naliendele) kilichopo mkoani Mtwara inatarajiwa kuanza kuingizwa mashambani.

" Miche hiyo ambayo ni ya muda mfupi ni bora na inatarajiwa kuuzwa kwa wakulima wa maeneo ya jirani kwa bei nafuu," alisema Luteni kanali Malechela.

Alitoa wito kwa wakulima wa krosho na wananchi wengine wanao tamani kuanza kuzalisha zao hilo walio maeneo ya jirani na kitalu cha Mkiwa, hasa wananchi wa mkoa wa Singida na mikoa jirani na Singida wachangamkie miche hiyo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...