Katika ishara ya kuonesha mabadiliko ya kisiasa ya mtu ambaye wakati mmoja alikuwa ametengwa, Rais wa Eritrea Isaias Afwerki amemesimama na mshirika wake mkuu, mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel na Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, kwa kuwapatia wanajeshi wake msaada waliohitaji kupigana na vikosi vya Tigray People's Liberation Front (TPLF) katika jimbo la Tigray.
Katika hotuba ya hivi karibuni katika bunge la Ethiopia, mshindi huyo wa Tuzo ya Amani Nobel alifichua kwamba Eritrea, iliwapa chakula, mavazi na silaha wanajeshi wa Ethiopia ambao walikuwa wamerudi nyuma wakati TPLF walipowashambulia mara ya kwanza na kuteka kambi zao mjini Tigray, eneo la Ethiopia ambalo linapakana na Eritrea.
Bw. Abiy alisema hatua hiyo iliwawezesha kurudi na kupigana na TPLF, vugu vugu la zamani la wapiganaji karibu 250,000, hadi lilipoondolewa katika utawala wa eneo hilo Novemba 28.
"Watu wa Eritrea wametuonesha... kuwa ni jamaa zetu kwa kusimama nasi wakati mgumu," aliongeza kusema.

No comments:
Post a Comment