Arsenal wamempeana mchezaji nyota wa Ujerumani Mesut Ozil, 32, kwa Juventus kwa mkopo wa miezi sita na wako tayari kupunguza marupurupu yake kuhakikisha ofa hiyo inafanikishwa. (Tuttosport via the Sun)
Manchester United wamejiondoa katika kinyang'anyiro cha kumsaka mlinzi wa Bayern Munich David Alaba, ambaye huenda akapatikana kwa uhamisho wa bure msimu ujao. Klabu hiyo ya The Old Trafford inahoji bei ya kiongo huyo raia wa Austria aliye na umri wa miaka 28 ambaye anacheza safu ya kushoto na nyuma. (The Athletic via Manchester Evening News)
Arsenal wana matumaini ya kuzipiku Manchester City na Bayern Munich katika mbio za kupata saini ya Tariq Lamptey, 20, kutoka Brighton, ikiwa iHector Bellerin, 25, ataamua kurejea katika klabu yake ya utotoni ya Barcelona. (Daily Mirror)
Kiungo wa kati wa Uholanzi Georginio Wijnaldum, 30, ataamua kuhusu ofa ya kurefusha mkataba wake Liverpool katika muda wa siku chache zijazo. (the Guardian)
Watford wameanza mazungumzo na klabu ya Villarreal ya Uhispania kuhusu uuzaji wa Etienne Capoue, inasemekana kuwa inatafuta £4m kumwachilia kiungo huyo wa kati raia wa Ufaransa wa aliye na umri wa miaka 32. (Daily Mail)
Mkufunzi wa West Ham United David Moyes ana matumaini kuwa kiungo wa kati wa England Declan Rice, 21, anaweza kushawishiwa asikubali kujiunga na Chelsea kwa kupewa mkataba mpya Olympic Stadium. (Daily Mail)
Juventus wanafikiria uhamisho wa Januari ili kumnasa kiungo wa zamani Paul Pogba kurudi Turin, lakini watahitaji Manchester United kukubali dauni la pauni milioni 50 kwa mchezaji huyo wa miaka 27.(Eurosport)
Paris St-Germain iko tayari kuipatia Inter Milan kiungo wake wa kati wa Argentina mwenye umri wa miaka 26 Leandro Paredes ili kubadilishana na kiungo wa Denmark Christian Eriksen, 28 (Le10Football - in French)
Meneja wa zamani wa Liverpool na Newcastle Rafael Benitez anaweza kuwa mkufunzi mpya wa Arsenal ikiwa klabu hiyo itaamua kumtema Mikel Arteta. (Sunday Express)

No comments:
Post a Comment