Search This Blog

Saturday, December 5, 2020

Ivory Coast yamrudishia hati za usafiri rais wa zamani Laurent Gbagbo


Ivory Coast imempa hati za kusafiri aliyekuwa rais wa nchi hiyo Laurent Gbagbo, na kumruhusu kurudi nyumbani kutoka uhamishoni Ubelgiji kabla ya mwaka kumalizika. 

Wakili wake Habiba Toure ametowa taarifa hiyo jana na kusema kwamba kiongozi huyo wa zamani ameshapokea hati mbili za usafiri, moja ya kidiplomasia na moja ya kiraia akiwa mjini Brussels na atarudi Ivory Coast kabla ya mwaka kumalizika. 

Hatua hiyo imechukuliwa baada ya kiongozi huyo wa zamani kufutiwa mashtaka katika kesi ya uhalifu wa kivita iliyokuwa ikimuandama kwenye mahakama ya kimataifa ya jinai ya ICC. 

Gbagbo amepokea hatua hiyo kama ishara ya maridhiano kutoka kwa rais Alassane Outtara ambaye mvutano wake mkali na wapinzani kuhusu kuchaguliwa kwake kwa muhula wa tatu umezusha masuali juu ya uthabiti wa nchi hiyo ya Afrika Magharibi uliopatikana kwa kazi ngumu.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...