Search This Blog

Tuesday, December 8, 2020

Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Kufungua Sekondari 4 Mpya januari


Na Faruku Ngonyani, Mtwara.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mtwara Bi. Erica  Yegella Tarehe 07 Disemba, 2020 amewaeleza  Madiwani lengo la Halmashauri hiyo kufungua Shule 4 za Sekondari ifikapo Januari 2021 kwa lengo la kupunguza kero ya kutembea umbali mrefu kwa Wanafunzi.

Ameyasema hayo katika Kikao Cha Baraza la Madiwani wakati akitoa utangulizi wa uwasilishaji wa taarifa ya utekelezaji uliofanyika kipindi chote ambacho Madiwani hao hawakuwepo Mara baada ya kuvunjwa kwa Baraza mwishoni mwa Mwezi Juni 2020 ili kupisha mchakato wa Uchaguzi Mkuu uliofanyikatarehe 28 Oktoba 2020.

Akiendelea kutolea ufafanuzi wa ujenzi wa Shule hizo, Bi. Yegella ameeleza kuwa vifaa mbalimbali vimeshakwenda katika maeneo ya ujenzi ambapo mafundi wapo kazini na vingine vinaendelea kupelekwa kwa kadri vinapohitajika lengo likiwa kumalizika kwa wakati.

Aidha amezitaja shule hizo ni paomoja na Sule ya Sekondari ya Tangazo, Lipwidi, Msangamkuu na  na Shule ya Sekondari ya MangoPachanne.

Lakini piaMkurugenzi huyo ametumia fursa hiyo kwa kuwaomba Madiwani hao kuendeleza nguvu ya uhamasishaji ili kufanikisha utekelezaji wa Ilani na Mipango ya maendeleo kwa Wananchi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...