Search This Blog

Wednesday, December 30, 2020

China yawasilisha ndege 14 za kivita Pakistan


Jeshi la Anga la Pakistan (PAF) limepokea ndege 14 za kivita aina ya "JF-17 Thunder Block II" zilizotengenezwa kwa ushirikiano na China.

Kamanda wa Jeshi la Anga la Pakistan Jenerali Mujahid Anwar na Balozi wa China mjini Islamabad Nong Rong, walihudhuria hafla iliyoandaliwa kwa ajili ya uwasilishaji wa ndege za kivita kwa PAF zilizotengenezwa kwa ushirikiano kati ya utawala wa Islamabad na Beijing.

Katika taarifa aliyotoa Anwar, aliipongeza Taasisi ya Anga ya Pakistan Complex (PAC) na Kampuni ya Kitaifa ya Usafirishaji  wa Anga ya China (CATIC), ambayo ilifanya kazi pamoja katika ujengezaji wa ndege hizo, akisisitiza kuwa uwasilishaji wa ndege  ulikuwa hatua muhimu kwa Pakistan.

Kwa sasa nchi hiyo ina ndege zaidi ya 900 za kivita.

Kwa upande mwingine, jaribio la kombora la ardhini kwenda angani lilifanyika kwa mafanikio na ushiriki wa Admiral Amjad Han Niyazi ambaye ni Kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Pakistan.

Niyazi alitoa taarifa kuhusu shughuli hiyo na kusema kwamba Jeshi la Wanamaji la Pakistani lina uwezo wa kujibu ipasavyo kwa aina zote za vitisho na uchokozi.

Maelezo zaidi juu ya sifa za kiufundi za kombora hilo hayakutolewa.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...