"Politburo" ya China, chombo cha juu chenye kufanya maamuzi ya chama kimesema uongozi wa chama hicho ulitekeleza jukumu muhimu la kupambana na janga la virusi vya Corona mwaka huu.
Nchi hiyo ya Mashariki mwa Asia imefanikiwa kwa kiwango kikubwa kudhibiti kusambaa kwa ugonjwa wa Covid-19 na imekuwa moja ya nchi iliyoripoti ukuaji wa uchumi mwaka huu licha ya nchi nyingi duniani kuathirika kiuchumi.
Hata hivyo, China ilishtumiwa vikali kwa kutotoa taarifa sahihi juu ya mlipuko wa virusi vya Corona, vinavyoaminika kuanzia katika mji wa kibiashara wa Wuhan mnamo mwezi Disemba mwaka uliopita.
No comments:
Post a Comment