Search This Blog

Monday, December 14, 2020

Amber Lulu amvaa Uchebe kisa mimba


Msanii Amber Lulu amemjibu mfanyabiashara Uchebe kwa kumwambia amkome na asitafute kiki kupitia yeye baada ya Uchebe ku-post picha kwenye mtandao wa Instagram akiwa na msanii huyo kisha kuandika 'mama kijaa' akimaanisha kwamba ni mjamzito.

Akiijibu post hiyo kupitia mtandao huo huo wa Instagram Amber Lulu ameandika kuwa "Uchebe tuheshimiane usilete miamko yako nitakuvurugaa, mambo ya kijinga sitaki kama unatafuta kiki sio kwangu, mama kijacho hiyo mimba umenipa wewe kaa kwa kutulia kaka koma tena koma, nina mnyamwezi wangu halafu namuelewa kichizi so please".

Kwa muda mrefu sasa msanii huyo wa BongoFleva anadaiwa kuwa na ujauzito lakini yeye mwenyewe bado hajaweka wazi kama kweli ni mjamzito na haijajulikana ni nani aliyempa ujauzito huo.

 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...