Search This Blog

Monday, November 16, 2020

Zari athibitisha kuachana na king bae wake

 


Mrembo na Mwanamama Zari amethibitisha kuachana na mwanaume wake aliyemtambulisha mtandaoni kama ‘King Bae’ ambaye alifikia hadi hatua ya kumvisha pete ya uchumba.

Ikumbukwe, mara baada ya Zari kuachana na Diamond Februari mwaka 2018, na hii ni baada ya #Zari kutangaza jambo hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, kwamba msanii huyo amekuwa akimsaliti kwa kuwa na wanawake wengine, #Zari alikaa kwa muda kidogo ndipo akaweka wazi kuwa kwenye mahusiano na mwanaume huyo ambaye hakuwahi kumuonyesha Sura.

Akizungumza na Wasafi TV mwishoni mwa Wikiendi, #Zari amesema kuwa ni kweli mwanaume huyo alikuwepo na wala haikuwa kiki lakini kuna vitu kati yao vilitokea hadi kupelelea mahusiano yao kuvunjika.

Kwa takribani wiki moja sasa #Zari amekuwa kwenye headsline upande wa stori za burudani hapa nchini kutokana na ujio wake na watoto wake, #Tiffah na #Nillan aliowaleta kumuona baba yao mzazi, msanii Nasib Abdul @diamondplatnumz.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...