Search This Blog

Thursday, November 19, 2020

Waziri Mkuu wa Pakistan Khan aanza ziara yake Afghanistan


Waziri Mkuu wa Pakistan Imram Khan aliwasili Kabul leo kukutana na Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani, katika wakati ambao mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Afghanistan na wawakilishi wa Taliban yamekwama na machafuko yanaongezeka. 

Ni ziara ya kwanza ya nchini Afghanistan tangu kuingia madarakani miaka miwili iliyopita. Ni ziara ya kiongozi wa ngazi ya juu kabisa wa Pakistan mjini Kabul tangu mazungumzo ya amani yalipoanza kati ya Taliban na serikali ya Afghanistan mjini Doha, Qatar. 

Na inakuja siku chache baada ya wizara ya ulinzi ya Marekani kutangaza kuwa itapunguza idadi ya wanajeshi wake nchini Afghanistan kutoka 4,500 hadi 2,500 ifikapo katikati ya Januari mwakani.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...