Waziri Mkuu wa Japan Suga Yoshihide, alisema kuwa anatarajia kuimarisha ushirikiano kati ya nchi mbili kufuatia uteuzi wa kiongozi wa chama cha Democrats Joe Biden kama rais wa 46 wa nchi ya Marekani baada ya kushinda uchaguzi wa Novemba 3.
Akiongea na waandishi wa habari na kumpongeza Biden, Suga alisema kuwa Japan na Marekani ni "nchi mbili za ushirika" ambazo zinazingatia maadili ya kimsingi ya uhuru na demokrasia.
Suga alisema, "Kwa moyo wote nampongeza Biden na (Makamu wa Rais Kamala) Harris. Ningependa tufanye kazi pamoja ili kuimarisha ushirikiano kati ya Japan na Marekani katika suala la kuboresha maadili ya ulimwengu na kuhakikisha ustawi na amani kwa washirika wa Indo-Pacific."
Katika ujumbe wake uliochapishwa kwenye akaunti ya mtandao wa kijamii wa Twitter, Suga pia alisema,
"Ningependa kushirikiana na nyinyi ili kuimarisha zaidi muungano wa Japan na Marekani."

No comments:
Post a Comment