Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdoğan amezungumzia udugu kati ya Uturuki na Azerbaijan na kwamba nchi yake itaendelea kusimama pamoja na wananchi wa Azerbaijan.
Erdoğan ameyazungumza hayo katika siku ya bendera ya taifa la Azerbaijan na Uturuki.
"Kwa mioyo na mali zetu zote, tunaunga mkono mapambano ya Azerbaijan ya kukomboa ardhi yake huko Nagorno-Karabakh, ambayo imekuwa chini ya uvamizi wa Armenia kwa karibu miaka 30 licha ya maamuzi ya Umoja wa Mataifa (UN) na Shirika la Usalama na Ushirikiano barani Ulaya (OSCE). Imani yetu na matumaini ya ushindi kamili imeongezeka hata zaidi.", alisema kiongozi huyo.
Uturuki imeahidi kuendelea kuinga mkono Azerbaijan katika mapambano yake dhidi ya Azerbaijan.
Erdoğan alimalizia kwa kuwaombea rehma za Mwenyezi Mungu wale wote waliopoteza maisha katika mapambano hayo.

No comments:
Post a Comment