Search This Blog

Thursday, November 12, 2020

Watu 7 wafariki kwenye ajali ya helikopta iliyotokea katika eneo la Sinai Misri


Watu 7 wameripotiwa kufariki kutokana na ajali ya helikopta iliyokuwa imebeba timu ya kikosi cha ukaguzi wa kitaifa, iliyotokea katika eneo la Peninsula ya Sinai nchini Misri.

Kulingana na taarifa zilizotolewa na kituo rasmi cha redio cha KAN kutoka Israel kinachotangaza kwa lugha ya Kiarabu, iliarifiwa kuwa helikopta iliyokuwa imebeba timu ya kikosi cha ukaguzi wa kitaifa ilianguka katika maeneo ya karibu na mpakani mwa Saudia Arabi ana Jordan.  

Taarifa zaidi zimefahamisha kufariki kwa watu 7 kwenye ajali hiyo ingawa watu hao hawakubainishwa uraia wao.

Mamlaka za Misri na Israel hazikutoa maelezo zaidi kuhusiana na ajali hiyo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...