Search This Blog

Monday, November 16, 2020

Watoto 4,000 wana kisukari Tanzania


Imebainika kuwa watu wengi wanaishi na ugonjwa wa sukari bila kujijua, hivyo wataalamu wameshauri wananchi kujenga tabia ya kupima afya zao ili waweze kukabili ugonjwa huo.

Aidha,  rekodi za Chama cha Wagonjwa wa Kisukari Tanzania (TDA), zinaonesha zaidi ya watoto 4,000 wanaishi na kisukari huku kikitaja ugonjwa huo kuwa ni tatizo kubwa kutokana na idadi ya watu kuongezeka.

Meneja wa TDA, Happy Nchimbi amesema  ili kupata takwimu hizo, chama kimekuwa kikiangalia vituo au kliniki ambazo zipo kwenye hospitali za mikoa zilizoanzishwa kwa jitihada za chama kusaidia watoto baada ya kugundulika kwamba wao pia wanapata kisukari.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...