Search This Blog

Sunday, November 1, 2020

Watano wafa katika vurugu za uchaguzi Cote d'Ivoire

 


Watu watano wameuwawa na wengine kadhaa kujeruhiwa baada ya vurugu kuzuka katika siku za uchaguzi nchini Cote d'Ivoire. Maafisa wanasema vurugu hizo zimetokea katika ngome za upinzani nchini humo. 

Zoezi la upigaji kura lilifanyika jana katika uchaguzi ambao, Rais Alassane Ouattara anawania muhula wa tatu, ambao pia upande wa upinzani unasema unafanyika kinyume na katiba. Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kutolewa baadaye leo. 

Tangu Agosti takribani watu 30 wameuwawa katika vurugu hizo za kabla ya uchaguzi, na kuzusha hofu ya kujirudia tena kwa vurugu za 2010-2011, ambazo zilisababisha vifo vya takribani watu 3,000, pale ambapo rais wa kipindi hicho Laurent Gbagbo, alipogoma kuukubali ushindi wa Ouattara. Ouattara ameomba wito wa utulivu.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...