Search This Blog

Sunday, November 1, 2020

Lindi Mwambao yauza kilo 1,404,59 za korosho ghafi

 



Na Ahmad Mmow, Lindi. 

Kilo 1,404,159 ambazo ni sawa na tani 1,404 na kilo 159 za korosho ghafi zimeuzwa na chama kikuu cha Ushirika cha Lindi Mwambao kupitia mnada wa nne kwa chama hicho kwa msimu wa 2020/2021.

Katika mnada huo ambao ni wasaba katika mkoa wa Lindi kwa msimu wa 2020/2021 ambao ulifanyika jana katika kijiji cha Madangwa, Halmashauri ya Mtama bei ya juu ilikuwa shilingi 2,388. Wakati bei ya chini ilikuwa shilingi 2,328 kwa kila kilo moja.

Katika ghala la BUCCO lenye tani 398 na kilo na kilo 143 za daraja la kwanza bei ya juu ni shilingi 2,388 na bei ya chini ni shilingi 2,352 ambazo zimenunuliwa na kampuni za SIBATANZA na BUDHAN.

Aidha katika ghala la Hazina(Mtama) ambalo lina tani 225 na kilo 944 ambazo zimenunuliwa na kampuni ya SIBATANZA, bei ya juu ni shilingi 2,348 na bei ya chini ni shilingi 2,328. Ambapo katika ghala la Ilulu (Mtama) kampuni za SIBATANZA na Export Trading Ltd zimefanikiwa kununua tani zote 393 na kilo 709 zilizopo katika ghala hilo kwa bei ya juu ya shilingi 2,388 na bei ya chini ni shilingi 2,380 kwa kila kilo moja. 

Mbali na maghala makuu hayo, lakini pia kampuni ya BUDHAN imenunua 314 na kilo 89 zilizopo katika ghala la Nangurukuru kwa bei ya shilingi 2,361.

Akizungumza baada ya wakulima kukubali kuuza kwa bei hizo, meneja mkuu wa chama kikuu hicho, Nuurdin Swallah alisema jumla ya shilingi 7,303,257,714 zimeingizwa na wanunuzi kwenye akaunti Ya Lindi Mwambao ambazo watalipa wakulima ambao korosho zao zilinunuliwa katika mnada wa tatu. Huku akiweka wazi kwamba Shilingi 288,512,360 zitaingizwa wakati wowote ili kukamilisha Jumla ya shilingi 7,591,770,074 ambazo ni malipo ya tani 3,180 na kilo 884 zilizonunuliwa katika mnada huo wa tatu. 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...