Search This Blog

Friday, November 13, 2020

Wanamgambo wa kundi la Taliban watekeleza shambulizi kwenye kambi ya jeshi nchini Afghanistan


Walinzi wa usalama 12 wameripotiwa kupoteza maisha kwenye shambulizi lililotekelezwa na wanamgambo wa kundi la Taliban katika mkoa wa Kunduz nchini Afghanistan.

Kulingana na taarifa za shirika la Toto News, mkuu wa halmashauri ya mji wa Kunduz Muhammed Yusuf Ayyubi alitangaza kushambuliwa kwa kambi ya kijeshi ya Bala Hisar na wanamgambo, iliyoko katika wilaya ya Imam Sahip.

Ayyubi aliongezea kusema kuwa walinzi wa usalama 12 walipoteza maisha na wengine 11 walijeruhiwa kwenye shambulizi hilo.

Wanamgambo wasiopungua 7 wa kundi la Taliban pia wameweza kuangamizwa.

Wizara ya Ulinzi ilitoa maelezo na kuarifu kwamba askari 4 walifariki na wengine 5 walijeruhiwa kufuatia shambulizi la bomu lililotekelezwa kwa kutumia gari kwenye wilaya ya Pagman iliyoko magharibi mwa mji mkuu wa Kabul nchini humo.

Hakuna yeyote aliyedaiwa kuhusika na shambulizi hilo.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...