Afya ya Rais wa Ukraine aliyepatwa na corona imeripotiwa kuendelea vizuri.
Zelenskiy ameandika katika ukurasa wake wa Facebook kwamba amepata afya njema katika hospitali anayotibiwa.
Akikumbushia kwamba amekuwa katika karantini kwa siku tatu, Zelenskiy, amesema,
"Nimejitenga lakini bado naendelea na kazi yangu. Natimiza majukumu yangu. Vyombo vyote vya serikali vinaendelea kufanya kazi kawaida. Siku hizi ninafanya mikutano yangu mtandaoni."
Zelenskiy alikutwa na corona mnamo Novemba 9.

No comments:
Post a Comment