Search This Blog
Friday, November 6, 2020
Walimu Wawili Kortini tuhuma za mauaji ya mwanafunzi
Walimu wawili wa Shule ya Awali na Msingi ya Holly Cross Nursery iliyopo Temeke jijijini Dar es Salaam wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakikabiliwa na shtaka la kudaiwa kumuua mwanafunzi wa Shule hiyo, Cathbert Chawe.
Washtakiwa hao ni, Leahdorice Agunda(35) na Maths Laizer ambaye ni Mkazi wa Mtoni Kijichi.
Wakisomewa hati ya mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi,Wankyo Simon mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu,Yusto Ruboroga amedai kuwa washtakiwa wanakabiliwa na shtaka moja ambao mnamo Septemba 14, 2020 katika shule ya awali na Msingi ya Holly Cross Nursery iliyopo maeneo ya Kijichi Wilaya ya Temeke wote Kwa pamoja wanadaiwa kumuua mwanafunzi wa shule hiyo, Cathbert Chawe huku wakijua kufanya hivyo ni kosa la kisheria.
Wankyo amedai kuwa upelelezi wa shauri Hilo bado haujakamilika na hivyo aliiomba mahakama hiyo ipange tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa.
Baada ya maelezo hayo Hakimu Ruboroga amesema washtakiwa hao hawarihusiwi kujibu chochote kwa kuwa kesi hiyo ni ya mauaji hivyo ameahirisha shauri hilo Hadi Novemba 19, mwaka huu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment