Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi wa Tobruk, washirika wa kisiasa wa Baraza Kuu la Libya na kiongozi wa kundi la silaha nchini Khalifa Hafter, walikubaliana juu ya utaratibu wa kufanya maamuzi ya mazungumzo yatakayofanyika Tunisia.
Wajumbe wa Libya walifanya mkutano wa mashauriano katika mji wa Buznika nchini Morocco hapo jana jioni, kama moja ya sehemu ya duru ya tatu ya mazungumzo.
Kulingana na taarifa iliyotolewa na Mohammed Abu Suneyne ambaye ni mwanachama wa Baraza Kuu la Nchi ya Libya, iliarifiwa kuwa wahusika wote walijadili suala la "usimamizi wa mchakato wa mazungumzo ya kisiasa nchini Tunisia, taratibu za kisheria za uteuzi wa watu watakaoteuliwa kwa nyadhifa za juu katika bodi ya utendaji na namna mambo muhimu yatakavyopewa kipaumbele."
Katika taarifa hiyo, pia ilielezwa kuwa mkutano wa mashauriano ulijadili maandalizi ya mazungumzo yaliyopangwa kufanyika Tunisia na njia za maamuzi zilizokubaliwa.
Akiongea katika mkutano huo, Waziri wa Mambo ya Nje wa Morocco Nasser Burita, alisema kuwa nchi yake iko tayari kuunga mkono juhudi zilizofanywa kupata suluhisho la mzozo wa Libya.
Mnamo Septemba 6-10 na Oktoba 2-6, mikutano miwili tofauti ilifanyika katika mji wa Buznika, Morocco kati ya Baraza Kuu la Nchi ya Libya na wajumbe wa Baraza la Wawakilishi iliyoitwa "Mikutano ya Mazungumzo ya Libya".
Wahusika wote wa Libya wanatarajiwa kukutana Tunisia mnamo Novemba 9 ili kupata suluhisho la mzozo wa kisiasa.

No comments:
Post a Comment