Search This Blog

Tuesday, November 3, 2020

Upinzani Ivory Coast 'kuandaa uchaguzi mpya'


Upinzani nchini Ivory Coast umesema kuwa unaunda serikali ya mpito baada ya kususia uchaguzi wa urais Jumamosi kwa sababu ya uamuzi wa Rais Alassane Ouattara wa kuwania muhula wa tatu.

"Moja ya majukumu ya serikali ya mpito itakuwa kuandaa uchaguzi wa haki, uwazi na wenye kujumuisha kila mmoja", kiongozi wa upinzani Pascal Affi N'Guessan amesema.

Aliongeza kuwa baraza la taifa la mpito limeundwa ambalo litamteua aliyekuwa rais wa nchi hiyo Henri Konan Bédié, kuongoza serikali ya mpito ambaye pia ni kiongoni wa chama cha Democratic huko Ivory Coast.

"Kumuendeleza Bwana Ouattara kama kiongozi wa taifa kuna uwezekano mkubwa wa kusababisha vita vya ndani kwa ndani,” Bwana N'Guessan amesema.

Chama tawala kimeonya upinzani dhidi ya jaribo lolote la kusababisha vurugu nchini humo.

Takriban watu 9 wameuawa wakati wa uchaguzi, huku waandamanji wa upinzani wakijaribu kuzuia watu kupiga kura.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...