Search This Blog

Tuesday, November 3, 2020

Bobi Wine anatarajiwa kuteuliwa kuwa mgombea urais hii leo


Leo ni siku ya pili ya zoezi la uteuzi wa wagombea wa kiti cha urais nchini Uganda, ambapo mpinzani mkuu Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine anatarajiwa kuteuliwa.

Kwa mujibu wa mwandishi wa BBC Issaac Mumena, Bobi Wine anatarajiwa kuteuliwa majira ya asubuhi.

Kabla ya kutoka nyumbani kwake, Bobi Wine alisema kuwa atazungumza na vyombo vya habari na amekubali kwenda na watu 10 kama inavyotakiwa na Tume ya Uchaguzi ya Uganda.

Hata hivyo, inasemekana kwamba jeshi la polisi limezunguka ofisi za chama cha Bobi Wine cha National Unity Platform, NUP.

Pia hali ya usalama imeimarishwa katika mji wa Kampala na vitongoji vyake.

Hata hivyo, ofisi za chama kingine cha upinzani cha FDC pia zimezungukwa na jeshi la polisi, Mumena anaeleza.

Chama cha FDC kimesema kwamba hakifuata masharti ya tume ya uchaguzi ya kwenda na watu 10.

Tamko la chama hicho limetolewa licha ya jeshi la polisi jana usiku kusema kuwa liko tayari kukabiliana na yeyote atakayekiuka masharti ya tume ya uchaguzi.

Hapo jana rais Yoweri Museveni alikuwa miongoni mwa walioteuliwa na kupata fursa nyingine ya kutetea kiti chake kwa muhula mwingine.





No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...