Aliyekuwa mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha Demokrasia Chadema Tundu Lissu amekamatwa na kuachiliwa baada ya kuhojiwa.
Kulingana na mtandao wa Twitter wa chama cha upinzani Chadema kiongozi huyo alikamatwa na jeshi la polisi.
Tundu Lissu amekamatwa nje ya jengo la ofisi za ubalozi wa Ujerumani, Uholanzi, Uingereza na Umoja wa Ulaya (EU) nchini Tanzania.
Hata hivyo polisi haijatoa tamko lolote kuhusu kukamatwa kwake .

No comments:
Post a Comment