Search This Blog

Monday, November 2, 2020

Lori laingia sokoni na kuua watu 20 nchini Nigeria


Watu 20 wameripotiwa kupoteza maisha kwenye ajali iliyotokea magharibi mwa Nigeria.

Kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya kitaifa,  iliarifiwa kuwa lori moja liliingia sokoni kwenye eneo la Akungba Akoko lililoko mkoani Ondo na kukanyaga umati.

Watu 20 walipoteza maisha na wengine wengi kujeruhiwa katika ajali hiyo.

Majeruhi walifikishwa katika hospitali za karibu kwa ajili ya matibabu.

Bado kuna hali ya wasiwasi kuhusiana na idadi ya vifo inayohofiwa kuongezeka.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...