Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy anatarajiwa kukabiliwa na mashtaka leo mahakamani mjini Paris, kwa shutuma za ufisadi na ushawishi usiofaa.
Anadaiwa kujaribu kupata siri za uchunguzi kutoka kwa wakili mkuu katika mahakama ya juu ya rufaa kupitia wakili wake mnamo mwaka 2014.
Wakili wake wa muda mrefu Thierry Herzog pia anakabiliwa na mashtaka.Ikiwa madai dhidi yao yatathibitishwa, basi wanaweza kupewa kifungo cha hadi miaka 10 jela.
Mashtaka hayo yanayotarajiwa kudumu hadi Disemba 10, yanachukuliwa kuwa si ya kawaida katika historia ya Ufaransa.
Hii itakuwa mara ya kwanza kwa rais wa nchi hiyo kusimama kizimbani akikabiliwa na mshtaka makubwa kama hayo nchini humo.

No comments:
Post a Comment