Search This Blog

Monday, November 23, 2020

Netanyahu alikutana na Mohammed bin Salman kisiri Saudi Arabia


Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alifanya ziara ya kisiri nchini Saudi Arabia jana Jumapili, na alikutana na mrithi wa mfalme Mohammed bin Salman, na pia waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani Mike Pompeo.

 Hayo yameripotiwa leo na kituo cha redio cha umma (Kan) cha Israel na pia kituo cha redio cha jeshi.Hata hivyo, ofisi ya Netanyahu pamoja na ubalozi wa Marekani mjini Jerusalem hazikutoa taarifa ya moja kwa moja kuhusu ziara hiyo.

 Gazeti la Haaretz la Israel lilichapisha picha kutokana na data za kufuatilia usafiri wa angani, zilizoonesha ndege binafsi iliyosafiri kutoka Tel Aviv hadi Neom ambako Bin Salman na Pompeo walipangiwa kukutana Jumapili. 

Pompeo amekuwa akijaribu kuishawishi nchi hiyo ya ghuba kuzifuata nchi jirani za Umoja wa Falme za Kiarabu na Bahrain katika kuboresha mahusiano na Israel, hatua inayojengwa haswa kwenye msingi wa wasiwasi dhidi ya Iran.

Saudi Arabia bado imekataa kurudisha uhusiano wao na Israel ikisema suala la utaifa wa Palestina linapaswa kushughulikiwa kwanza.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...