Mtu mmoja ameripotiwa kutekeleza jaribio la shambulizi kwenye jengo la ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutumia gari katika mji mkuu wa Berlin nchini Ujerumani.
Gari la mshambuliaji huyo lililokuwa na maneno yanayosoma, "Makatili wa watoto na wazee waliolaaniwa" na "Komesheni sera za utandawazi", liligonja vizuizi vya chuma vya lango kuu na kusimama nje ya jengo la ofisi ya Waziri Mkuu nyakati za asubuhi.
Baadaye dereva wa gari hilo aliingiliwa na polisi.
Wakati wa utekelezaji wa jaribio hilo la shambulizi, Waziri Mkuu Angela Merkel alikuwa akiendesha mkutano wa baraza la mawaziri.

No comments:
Post a Comment