Wananchi wamefurahi baada ya Manuel Merino kutangaza kujiuzulu ikiwa ni siku chache tangu kuchaguliwa baada ya Bunge kumtoa Madarakani Rais Martin Vizcarra
Merino alitangaza uamuzi huo kwenye Runinga na kusema ni kwa ajili ya maslahi mapana ya Taifa. Tayari Mawaziri 9 kati ya 18 wamejiuzulu kufuatia vifo vya watu 2 vilivyotokana na mvutano baina ya Polisi na waandamanaji
Mtandao wa #HakiZaBinadamu umesema watu 112 wameumizwa huku wengine 41 wakiwa hawajulikani walipo. Waziri Mkuu wa #Peru, Antero Flores-Araoz amesema Vizcarra ameondolewa kwa mujibu wa Sheria
No comments:
Post a Comment