Binti mkubwa wa rais wa zamani wa Ghana Jerry Rawlings ametoa onyo dhidi ya wezi wa mtandaoni wanaodai kuwa wanachangisha pesa kwa ajili ya mazishi ya baba yake.
Katika taarifa yake aliyoituma kwenye mtandao wa Facebook siku ya Alhamisi Zanetor Rawlings, alisema akaunti gushi za mitandao ya kijamii zimebuniwa kwa ajili ya kukusanya pesa
Amesema kuwa wezi wanawalenga wale wanaomtumia salamu za rambirambi kufuatia kifo cha baba yake.
Bi Rawlings ni mbunge wa jimbo la Klottey Korle katika bunge la Ghana.

No comments:
Post a Comment