Watu 9 akiwemo afisa mmoja wa polisi wameripotiwa kupoteza maisha kwenye ghasia zilizozuka kote nchini wakati wa kuhesabu kura za uchaguzi wa rais uliofanyika siku ya Jumapili nchini Guinea.
Kulingana na taarifa za vyombo vya ndani ya nchi, iliarifiwa kuanzishwa kwa ghasia katika ya vikosi vya usalama na waandamanaji tangu siku ya Jumatatu, kufuatia maelezo yaliyotolewa na chama cha RPG kinachoongozwa na rais wa sasa Alpha Conde.
Ghasia hizo zilizozuka kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama, zilisababisha vifo vya watu 9 ambapo 6 waliuawa kwa silaha.
Mojawapo ya watu waliopoteza maisha kwenye ghasia hizo amebainishwa kuwa afisa wa polisi aliyeuawa kwa kupigwa na umati.
Cellou Dalein Diallo, ambaye ni kiongozi wa chama cha UFDG na mgombea urais aliyekuwa mpinzani wa karibu Conde, alidai kuwa watu 16 waliuawa.

No comments:
Post a Comment