Search This Blog

Thursday, October 22, 2020

Bunge la Uhispania lapinga muswada wa kutaka kuiondoa serikali madarakani


Muswada uliowasilishwa bungeni na chama cha Vox tangu mwezi Januari kwa ajili ya kuindoa serikali ya Uhispania madarakani , imeripotiwa kupingwa na wawakilishi wa bungeni.

Bunge la Uhispania lilifanya vikao kwa siku mbili kwa ajili ya kupiga kura, ambapo wanachama 52 wa Vox pekee ndio waliopiga kura ya ‘nido’ huku wanachama 298 wa vyama vingine wakapiga kura ya ‘hapana’.

Muswada huo ulioletwa na chama cha Vox ambacho kinafahamika kwa sera za dhidi ya wahamiaji na waislamu, ulikuwa ukiipinga serikali na kuitaka kujiuzulu kwa madai ya kushindwa kukabiliana na janga la covid-19 nchini lililosababisha idadi kubwa ya vifo, na kujiunga na vyama vingine vya kisiasa ili kuhamasisha ubaguzi Catalonia na Basque.

Serikali ya chama tawala ambacho kimekuwa kikishutumu chama cha Vox kwa madai ya uchochezi wa chuki za kisiasa na ukiukaji wa haki za kidemokrasia na za kibinadamu, kimetolewa maoni ya kuwa na nguvu kwa hoja iliyokataliwa.

Wakati hoja hiyo ya kuindoa serikali imewasilishwa bungeni kwa  mara ya 5 katika historia ya demokrasia ya Uhispania, ipo kanuni ya katiba inayozuia kuwasilishwa kwa hoja kama hii hadi mwezi Februari.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...