Search This Blog

Tuesday, October 6, 2020

Tetesi za soka kimataifa


 Manchester United imejiondoa katika kumsaini mshambuliaji wa England Jadon Sancho 20, baada ya kubaini kwamba uhamisho huo huenda ukaigharimu timu hiyo £227m kutokana na dau la £108m linalotakiwa na Borussia Dortmund , pamoja na mahitaji ya marupurupu ya mshahara kutoka kwa ajenti wake (Guardian)

West Ham walikuwa wako tayari kumsaini beki wa England Fikayo Tomori, 22, kwa mkopo ambao walikuwa wamejitolea kuilipa Chelsea dau la £50,000 kila mara alipokosa kuwachezea The Hammers , lakini makubaliano hayo hayakuafikiwa. (Talksport)

Tottenham na West Ham wana hamu ya beki wa kati wa Wales Joe Rodon, 22, na huenda wakawasilisha ombi la dau la £18m kabla ya siku ya mwisho ya ligi ya EFL mnamo tarehe 16. (Wales Online)

West Ham huenda ikawasilisha ombi la kumsajili beki wa Watford na England Craig Dawson, 30, lakini watahitajika kulipa £4m. (Sun)

Ombi la Manchester United la kumsajili winga wa Senegal Ismaila Sarr kwa kipindi kilichosalia cha msimu huu lilikataliwa na Watford , lakini inaweza kujaribu tena mwezi huu licha ya kwamba The hornets wanataka mkataba wa kudumu. (Manchester Evening News)

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uholanzi Georginio Wijnaldum amepuuzilia mbali hamu kutoka kwa klabu ya Barcelona . Kandarasi ya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 inakamilika msimu ujao katika uwanja wa Anfield. (Mirror)

Klabu ya Ufaransa ya Saint-Etienne imeikosoa Arsenal kwa kushindwa kumruhusu beki kinda wa Ufaransa William Saliba kurudi katika klabu hiyo. (Talksport)

Barcelona itasubiri hadi mwisho wa msimu wa 2021 ili kumsajili beki wa Uhispania Eric Garcia, 19, kutoka Manchester City. Barca ilitoa Yuro milioni 2 katika siku ya mwisho ya dirisha la uhamisho. (Marca)

Jaribio la Barcelona kumsaini mshambuliaji wa Lyon na Uholanzi Memphis Depay, 26, lilikatizwa baada ya winga wa Ufaransa Ousmane Dembele, 23, kukataa kuondoka Manchester United. (AS)

Watford na Middlesbrough inamtaka beki wa kushoto wa Chelsea na Ghana baba Rahman , 26, kwa mkopo wa muda mrefu . (Goal)



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...