Search This Blog

Wednesday, October 7, 2020

Lady Jaydee aitwa BASATA


Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano wa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Nago amesema kupitia Mwanasheria wao wamemtumia barua ya kutaka kuonana msanii mkongwe wa BongoFleva Lady Jaydee kuhusu wimbo wake ambapo inasemekana unahamasisha matumizi ya uvutaji bangi.

Kaimu Afisa Habari na Mawasiliano wa BASATA Godfrey Nago amefafanua zaidi kuhusiana na hilo ambapo amesema.

"Kuhusu taarifa hizo naweza kusema nusu zina ukweli na nusu hazina ukweli kwa sababu bado hatujaita mkutano au kuongea na mtu yeyote kwenye hadhara kuhusu suala hilo, kitu ambacho tumefanya ni kumuita yeye kwanza na tayari tumeshampelekea barua kupitia Mwanasheria wetu ambayo anatakiwa aripoti hapa, halafu kuanzia hapo ndiyo tutakuwa na cha kuzungumza naye, huwezi kutoa hukumu kabla hujamzikiliza mtu"



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...