Search This Blog

Sunday, October 18, 2020

Kilo 7,225,504 za korosho zanunuliwa RUNALI


Na Ahmad Mmow, Nachingwea.

Kilo 7,225,504 zimenunuliwa katika chama kikuu cha ushirika cha RUNALI kupitia mnada wa pili kwa msimu wa 2020/2021 katika chama hicho. 

 Katika mnada huo uliofanyika leo mjini Ruangwa kampuni 17 zilijitokeza kuomba kununua korosho hizo zilizopo katika maghala makuu sita yaliyopo katika wilaya za Liwale, Nachingwea na Ruangwa. Ambapo bei ya juu ilikuwa shilingi 2,438 na bei ya chini ni shilingi 2,301. Huku ikishuhudiwa bei 68 tofauti zikiombwa na kampuni hizo 17. 

 Katika mnada huo ni kampuni moja tu iliyoomba kununua kwa njia ya mtandao kupitia soko la bidhaa (TMX). Kampuni hiyo iliomba kununua tani 350 kwa bei ya shilingi 2,367 kwa kila kilo moja kutoka katika ghala la Lindi farmers lililopo wilayani Nachingwea. 

 Katika mnada huo ambao korosho zipo katika maghala sita bei ambazo zimetumika kununua korosho hizo ghala la Kilimani ( Nachingwea) bei ya juu ni shilingi 2,405 na bei ya chini ni shilingi 2,360 kila kilo moja, ghala la Lindi farmers (Nachingwea) bei ya juu 2,435 na bei ya chini 2,405, ghala la Pachani bei ya juu 2,438 na bei ya chini 2,376, ghala la Umoja ( Liwale ) bei ya juu ni 2,348 na bei ya chini2,301 na katika ghala Lipande (Ruangwa) bei ya juu ni shilingi 2,405 na bei ya chini 2,315. 

Akizungumza baada ya wakulima kuridhia bei hizo, mwenyekiti wa RUNALI, Hassan Mpako aliwatoa hofu wakulima kuhusu changamoto ya vifungashio.

 Alisema chama hicho kimejipanga vizuri msimu huu. Kwani mahitaji halisi ni gunia 600,000, ambapo tayari chama hicho kimepata gunia 400,000 ambazo ni robo tatu ya mahitaji kwa msimu huu wa 2020/2021. 

Huku akiwahakikishia kwamba ndani ya wiki mbili kiasi cha gunia zilizosalia(200,000) zitapatikana.  Aidha mwenyekiti huyo wa RUNALI aliwataka wakulima wanaodaiwa madeni ya pembejeo walipe haraka ili kuwatia moyo wakopeshaji waweze kukopesha tena. 

 Alisema wakulima wanatakiwa watambue tofauti ya msaada na deni. Kwahiyo hawana budi kulipa ili wajitengenezee uaminifu kwa wakopeshaji. 

 Katika hatua nyingine meneja mkuu wa chama hicho, Jahida Hassan alisema jumla ya shilingi 3.8 bilioni zimelipwa kwa wakulima wa zao hilo ambao  korosho zao zilinunuliwa katika mnada wa kwanza. 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...