Search This Blog

Wednesday, October 28, 2020

Bolivia yafutilia mbali agizo la kumkamata Rais wa zamani

Bolivia imetangaza kufutilia mbali agizo la kumkamata Rais wa zamani wa nchi Evo Morales lililotolewa Desemba 2019.

Jaji mkuu wa mahakama ya sheria ya mkoa wa La Paz Jorge Quino, alitoa maelezo kwenye kituo cha televisheni cha Unitel, na kutangaza kufutiliwa mbali kwa agizo la kumkamata Morales aliyekuwa akiandamwa na kashfa ya ghasia na ufadhili wa magaidi.

Quino alielezea kuwa baadhi ya madai hayo yalikuwa na makosa baada ya kufanyiwa uchunguzi wa kina, na kuonekana kumnyima Morales haki ya kujitetea kisheria.

Wakati huo huo, agizo la kumkamata Waziri wa zamani wa sheria Hector Arce kwa madai ya ulaghai kwenye uchaguzi wa tarehe 20 Oktoba 2019 pia lilifutiliwa mbali.

Hector Arce, mawaziri kadhaa pamoja na baadhi ya viongozi serikali wamekuwa katika ubalozi wa Bolivia nchini Mexico kwa kipindi cha mwaka mmoja sasa.


 



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...