Mwenyekiti wa CCM Mkoa Kagera Bi. Costancia Buhiye akimnadi Mgombea Ubunge Jimbo la Nkenge Frolent Kyombo Mara Baada ya Kumkabidhi Ilani ya CCM.
Mgombea Ubunge Jimbo la Nkenge Frolent Kyombo akimnadi sera za Ilani ya CCM na ahadi zake kwa wapiga Kura na Wananchi Jimbo la Nkenge.
Shangwe la Vijana wa CCM Jimboni Nkenge likiendelea wakati wa Uzinduzi wa Kampeini Jimboni humo.
Mgombea Ubunge Jimbo la Nkenge Frolent Kyombo akiwa amesimama Jukwaani na mkewe wakiomba Kura kwa Wananchi katika Jimbo la Nkenge wakati wa Uzinduzi wa Kampeini Jimboni humo.
Bi. Regina Zachwa Mbunge Mteule UWT Kagera akiomba Kura kwa wanajimbo la Nkenge Kura za kutosha kwa Rais, Mbunge na Madiwani lengo ni kazi ziendelee.
Wanajimbo la Nkenge wakiendelea kufuatilia Mkutano wa Uzinduzi wa Kampeini Jimboni humo.
====== ====== ====== =========
Na Abdullatif Yunus MichuTv.
Nkenge Ni Jimbo mojawapo Miongoni mwa majimbo Tisa yanayopatikana Mkoani Kagera, Jimbo hili likiwa na historia ya Kutawaliwa na Chama Cha Mapinduzi, na zaidi limeonekana kuendelea kutekeleza vyema Ilani zilizotangulia za Chama hicho.
Tayari mbio za kuomba Tena ridhaa ya kuendeleza mazuri na mema Jimboni humo zimeanza Rasmi baada ya Uzinduzi wa Kampeini katika Jimbo hilo kufanyika Septemba 6, 2020.
Mgombea Ubunge kupitia Chama Cha Mapinduzi Frolent Kyombo ndiye aliyepewa dhamana na Chama chake kupeperusha Bendera kutetea Jimbo la Nkenge, ambapo katika ahadi zake jukwaani ameahidi kuendelea na Kazi nzuri iliyofanywa na watangulizi wake, na kuboresha Yale mengine yaliyosalia Kama vipolo yakiwemo Masuala ya Barabara, Maji, Umeme na Mikopo.
Awali aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri ya Missenyi Jimboni humo Ndg. Projestus Tegamaisho ameeleza katika Uzinduzi huo kuwa, kwa kipindi kilichopita Halmashauri ya Missenyi imetekeleza Ilani kwa asilimia miamoja ikiwa Ni pamoja na utekelezwaji wa Miradi yote.
Aidha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa Kagera Bi. Costancia Buhiye katika salaam zake Kama mgeni rasmi amewaomba Wanachama wa CCM kuacha Makundi na kuongeza kuwa mchakato ulikuwa na watu wengi mahiri na shupavu, lakini Chama kimemrudisha Kyombo ndiye wa kwenda nae.
Akiomba Kura Kwa Wananchi hao Bi. Regina Zachwa Mbunge Mteule UWT Kagera, amewakumbusha Wananchi umuhimu wa kukipigia Chama Cha Mapinduzi Kura za kutosha ili kupata Wabunge wengi wakiwemo Wateule wa Viti Maalum ili kuleta chachu ya Maendeleo Jimboni Nkenge.

No comments:
Post a Comment