Search This Blog

Sunday, September 6, 2020

DK MSUYA: CCM MWANGA HAKUNA MAKUNDI, TUTAHAKIKISHA WAGOMBEA WETU WOTE WANASHINDA KWA KISHINDO


Charles James, Michuzi TV

ALIYEKUA mtia nia kupitia wa Ubunge Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro kupitia Chama cha Mapinduzi, Dk Ombeni Msuya amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli na mgombea Ubunge wa jimbo hilo, Joseph Thadayo.

Dk Msuya ametoa kauli hiyo alipofika kumnadi Thadayo katika kampeni za ubunge jimbo la Mwanga ambapo amesema yeye na wenzake 53 ambao waligombea pamoja na Thadayo wataendelea kumuunga mkono mgombea aliyepitishwa na chama.

Amesema yeye ni kijana aliyelelewa ndani ya CCM hivyo maamuzi yaliyotolewa na chama kumpitisha Thadayo anayaheshimu kwa sababu ni ya kidemokrasia na atatumia nguvu na akili zake kuhakikisha Jimbo la Mwanga linabaki CCM na wanaibuka na ushindi wa kura nyingi.

" Sisi bado ni vijana hivyo ni jukumu letu kuunganisha nguvu zetu wote ili tuweze kupata kura nyingi za mgombea wetu wa Urais, Dk John Magufuli, mgombea wetu wa Ubunge na Madiwani wote wa kata 20.

Rais wetu amefanya mambo makubwa sana, miradi aliyoianzisha ndani ya Nchi yetu imekua ajira kwa maelfu ya watanzania wenzetu, usafiri wa Treni huku Kaskazini tulishausahau lakini Dk Magufuli ameurudisha, hakika anastahili mitano tena," Amesema Dk Msuya.

Dk Msuya ambaye pia ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dodoma amesema CCM Wilaya ya Mwanga haina makundi na sasa akili yao ni kushinda kwa kishindo uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 28 mwaka huu.

" Hakuna makundi Mwanga, lengo letu ni moja tu kuhakikisha Dk Magufuli anapata kura za kishindo, mgombea wetu wa Ubunge anaibuka mshindi na Halmashauri yetu inaundwa na madiwani wa CCM, hivyo niwaombe wananchi wote Oktoba 28 tujitokeze kwa wingi tukawaoneshe wapinzani kwamba Nchi hii CCM ndo Baba lao," Amesema Dk Msuya.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge mstaafu wa Mwanga, Cleopa Msuya ambaye aliwasihi wana CCM wote kuungana na kushirikiana katika kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura na kueleza mafanikio yote yaliyofanywa na Rais Magufuli ndani ya kipindi chake cha miaka mitano.
 Aliyekua Mtia Nia wa Ubunge Jimbo la Mwanga mkoani Kilimanjaro na Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha UDOM, Dk Ombeni Msuya akizungumza katika mkutano wa kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwanga, Joseph Thadayo pamoja na kumuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli na madiwani wa kata 20 za Halmashauri hiyo.
 Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge Mstaafu wa Jimbo la Mwanga, Cleopa Msuya akimuombea kura Mgombea Urais wa CCM, Dk John Magufuli, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Mwanga, Joseph Thadayo na Madiwani wa Kata 20 za Halmashauri hiyo.
 Mgombea Ubunge Jimbo la Mwanga, Kilimanjaro, Joseph Thadayo akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni zake za Ubunge.


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...