Search This Blog

Thursday, September 17, 2020

Wamiliki wa pool table watakiwa kuyasajili wapate leseni


 Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania (GBT) imewataka wamiliki wote wa 'pool tables' kuhakikisha zinasajiliwa na kupatiwa leseni. Imeeleza taarifa iliyotolewa kwenye tovuti ya Bodi hiyo.

GBT yenye jukumu la kusimamia uendeshaji wa michezo ya kubahatisha hapa nchini imesema kuwa Kifungu Namba 52 cha Sheria ya Michezo ya Kubahatisha ya mwaka 2003 'pool table' zote zinatakiwa kusajiliwa ili kuwezesha uendeshaji wa mchezo huo kihalali.

Taasisi hiyo imesema kuendesha mchezo huo bila usajili ni kinyume sha sheria na hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaokaidi agizo hilo.




No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...