Man United inatumai kuwasajili wachezaji watatu kabla ya kukamilika kwa dirisha la uhamisho la msimu huu, huku mshambuliaji wa England na Borussia Dortmund Jadon Sancho 20 akisalia mchezaji wanayemlenga kwa udi na uvumba. (Manchester Evening News)
Uwezo wa mkufunzi wa Real Madrid Zinedine Zidane kukibadilisha kikosi chake kutategemea iwapo Man United itamsajili mshambuliaji wake Gareth Bale. (Marca - in Spanish)
Wawakilishi wa beki wa kushoto wa Porto na raia wa Brazil mwenye umri wa miaka 27 Alex Telles wamesafiri hadi Man United ili kuanza mazungumzo na United. (A Bola, via Metro)
Manchester City imemtambua beki wa Sevilla raia wa Brazil Diego Carlos, 27, na mchezaji wa klabu ya Atletico Madrid na raia wa Uruguay Jose Gimenez, 25, kama mbadala wa beki wa kati wa Napoli na Senegal Kalidou Koulibaly, 29. (Sport - in Spanish)
Aston Villa inataka kumsaini mchezaji wa England mwenye umri wa miaka 20 Rhian Brewster kutoka Liverpool for £20m. (Sun)
Klabu za ligi ya Premia zinaamini kwamba Brewster ataruhusiwa kuondoka Liverpool katika dirisha hili la mismu wa uhamisho huku klabu za Sheffield United na Crystal Palace pia zikiwa na hamu ya kumsajili mshambuliaji. (Telegraph - subscription required)
Barcelona ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara, 29 - ambaye analengwa na Liverpool kurudi katika klabu hiyo. (Bild - in German).
Thiago Alcantara
The Blues pia wana matumaini ya kuafikia makubaliano na Rennes baada ya kutoa dau la £20m kwa Mendy. (Mail)
Kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 29, angekuwa mchezaji anayelengwa na mkufunzi wa Inter Milan Antonio Conte lakini huenda akagharimu £60m. (Calciomercato - in Italian)
West Ham imejiandaa kutoa dau lililoimarika la £30m kumnunua beki wa Burnley na England James Tarkowski, 27. (Evening Standard)
Wolves inakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Porto Vitor Ferreira kwa mkopo wa muda mrefu msimu huu huku wakiwa na mbadala wa kumnunua kwa dau £18m. (Express and Star)
Arsenal huenda ikakabidhiwa fursa ya kumsajili beki wa Ghana na Atletico Madrid Thomas Partey, 27, huku klabu hiyo ya Uhispania ikihitaji fedha zaidi za kumnunua kiungo wa kati wa Espanyol na Uhispania Marc Roca 23. (Marca, via Mirror)
Chelsea imekataa kumuuza mchezaji wa Ufaransa Tiemou bakayoko kwa dau la chini ya £30m , huku AC Milan ikiwa haitaki kulipa zaidi ya £25m. (Gazetta dello Sport - in Italian)
Mkufunzi mpya wa Barcelona Ronald Koeman ameambia klabu hiyo anataka kumzuia Phillipe Coutinho msimu huu badala ya kumtoa mchezaji huyo wa Brazil kwa mkopo. (Marca)
Mchezaji wa Scotland Ryan Frazer 12 amekubali kujiunga na klabu ya Newcastle baada ya kuondoka klabu ya Bournemouth mwisho wa msimu na sasa anatarajiwa kufanyiwa vipimo vya matibabu. (Sky Sports)
Mkufunzi wa Manchester United Ole Gunnar Solskjaer amezungumza na winga wa England Jadon Sancho, 20, kuhusu kujiunga na klabu hiyo kutoka klabu ya Borussia Dortmund msimu huu . (Express)
Licha ya Gareth Bale kutaka kuondoka Real Madrid , klabu hiyo haijapokea maombi yoyote ya mshambuliaji huyo wa Wales, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 akikataa kupunguziwa mshahara wake na hivyobasi kuwazima wanaommezea mate. (Mundo Deportivo - in Spanish)
Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, 33, anatarajiwa kukalia mtihani wa Lugha siku ya Jumatatu ili kupatiwa uraia wa Itali , hatua itakayomfanya kukamilisha uhamisho wake kujiunga na Juventus.(Eurosport)
Mshambuliaji wa Bosnia Edin Dzeko, 34, ameomba kuondoka klabu ya Roma na kujiunga na Juventus. (Corriere dello Sport - in Italian)
West Ham italazimika kuongeza ombi lao la dau la £27m ili kuwa na fursa yoyote ya kumsajili beki wa kati wa Burnley James Tarkowski, 27. (Sun)
Tarkowski anasema kwamba anataka kucheza katika ligi ya mabingwa iwapo fursa itajitokeza na anatumai kurudi katika kikosi cha England. (Telegraph)
Sheffield United inakamilisha dau la £11m kumsaini beki wa Derby na England Jayden Bogle, 20, na Max Lowe, 23, na pia watampeana mshambuliaji wa Ireland Callum Robinson, 25, ili kumpata winga wa Usochi Oliver Burke, 23. (Mail)
Mchezaji wa Liverpool na aliyekuwa winga wa timu isiozidi wachezaji wa miaka 21 nchini England Sheyi Ojo, 23, anatarajiwa kujiung na klabu ya Cardiff katika ligi ya daraja la kwanza nchini England kwa mkopo licha ya hamu kutoka Nottingham Forest. (Liverpool Echo)

No comments:
Post a Comment