Na Ahmad Mmow, Lindi.
Mgombea ubunge katika jimbo la Lindi kwa tiketi ya chama cha Alliance for Change and Transparency (ACT-Wazalendo), Isihaka Mchinjita amehaidi kwamba akichaguliwa kuwa Mbunge atapambana ili kuhakikisha kwamba fedha za kodi ya usafirishaji mazao nje inarudi kwa wakulima wa korosho.
Mchinjita ametoa ahadi hiyo leo katika mtaa wa Nachingwea, manispaa ya Lindi alipozungumza na wananchi wa kata ya Nachingwea kwenye mkutano wa kampeni ya uchaguzi.
Alisema ili uzalishaji wa korosho uongezeke nchini ni jambo jema fedha za kodi ya usafirishaji mazao nje ambayo ilianzishwa na wakulima wa zao hilo ili kuongeza uzalishaji zinarudi kwa wakulima ili zifanye kazi iliyokusudiwa na wakulima hao.
Alisema anakila sababu ya kupambana ili fedha hizo zirejeshwe. Kwani kabla ya serikali kuingilia kati nakuchukua fedha hizo uzalishaji uliongezeka. Kwamada kwamba zilikuwa zinatumika kuzalisha miche, kununua pembejeo, viwatilifu na kugharamia utafiti wa zao hilo.
Alisema baada ya serikali kuchukua fedha hizo na hatimae kubadilisha sheria ya kodi hiyo uzalishaji umeshuka na kuchangia wakulima wa zao hilo kuwa na maisha magumu. Huku bei zake zikishuka na wakulima kutolipwa kwawakati.
" Nawapongeza akina Nape Nnauye, Hassan Masala, Hawa Ghasia, Bwege, Mwambe na Ahmad Khatani kwani walipambana sana kuhusu dhuluma hii. Serikali ili kuhalalisha kitendo chake cha kuchukua fedha za wakulima ilibadilisha sheria ambayo inahalalisha fedha hizo kuchukuliwa na serikali kuu," alisema Mchinjita.
Kutokana na hayo, mgombea ubunge huyo alisema akiingia bungeni kwakusaidiana na wabunge wenzake wenye uchungu na jasho la wakulima wa zao hilo atapambana ili kuhakikisha fedha hizo zinarejeshwa kwa wakulima wenyewe. Kwani ni zao pekee lenye kodi ya usafirishaji wa mazao nje.
Mchinjita alikwenda mbali kwakutoa suluhisho ambalo litamfanya aachie kudai fedha hizo ni serikali kuweka na kuchukua kodi ya usafirishaji mazao nje katika mazao mengine. Ikiwemo pamba kahawa na mengine ghafi yanayosafirishwa nje.
Aidha Mchinjita aliungana na mgombea wa urais kupitia chama hicho( Bernard Membe) ambaye katika uzinduzi wa kampeni kitaifa za Urais uliofanyika katika manispaa ya Lindi aliyesema kwamba wanunuzi wa korosho wanaojulikana kwa jina la kangomba watanunua zao hilo bila kubughuziwa iwapo atachaguliwa kuwa Rais.
Mchinjita ambae kitaaluma ni mwalimu alisema kangomba ni msaada mkubwa kwa wakulima wadogo ambao wanashindwa kumudu gharama za uendeshaji mashamba yao. Ikiwa nipamoja na uwezo wa kupalilia mikorosho, kununua viwatilifu na pembejeo. Kwahiyo kuwasumbua kangomba nikuwanyima msaada wakulima wadogo wasizalishe kwa wingi.
Kwaupande wake mgombea wa kiti cha udiwani wa kata hiyo ya Nachingwea, Doa Omari Doa alisema akichaguliwa nakuwa diwani wa kata hiyo atalivalia njuga tatizo la viwanja vya makazi katika kata hiyo ambalo limeshindwa kupata ufumbuzi kwa muda mrefu huku watu wengi wakiwa hawana viwanja wakati ina ardhi ya kutosha.

No comments:
Post a Comment