Search This Blog

Thursday, September 3, 2020

Manchester United yamsajili Donny van de Beek

 


Manchester United imefanikiwa kumsajili kiungo wa kimataifa wa Uholanzi, Donny van de Beek.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amejiunga na Mashetani Wekundu kwa ada ua uhamisho ya Pauni Milioni 40 kutoka kwa vigogo wa Uholanzi,  Ajax.

Van de Beek aliyesaini mkataba wa miaka mitano, wenye kipengele cha kuongezewa mwaka mmoja zaidi, inaaminika atakuwa analipwa mshahara wa Pauni 107,000 kwa wiki nje posho.

Anakuwa mchezaji mpya wa kwanza kusajiliwa na kocha Ole Gunnar Solskjaer kuelekea msimu ujao na anatarajiwa kuunda safu nzuri ya kiungo Old Trafford pamoja na Paul Pogba na Bruno Fernandes.    



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...