Search This Blog

Sunday, September 13, 2020

Cosmas Cheka ashinda mkanda wa UBO baada ya kumtwanga Mmalawi


Bondia wa Tanzania, Cosmas Cheka ameshinda pambano dhidi ya Mmalawi, Hannock Phiri lililofanyika Uwanja wa Jamhuri, Morogoro

Walipigana wa uzito wa Light kuwania UBO International Title ambapo pambano hilo lilikuwa la round 12. Kwa uamuzi wa majaji ameonekana kushinda japo mpinzani wake ameonekana kutokubaliana na uamuzi huo

Mbali na hayo, Cheka amesema kuwa kama mpinzani wake hajaridhika, arudie pambano na kwamba yeye yuko tayari kumfuata Malawi

Katika Mapambano ya utangulizi, Mwanadada Zulfa Macho, mtoto wa Yusuph Macho alishinda kwa Knock-Out kwenye round ya kwanza kwenye pambano dhidi ya Mmalawi, Ndau Chilimba



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...