Search This Blog

Sunday, August 2, 2020

Waziri Mpina ataka maonyesho ya nanenane kutumika kutatua chanamoto za wakulima, wavuvi na wafugaji

Na Farida Saidy, Morogoro.

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Luaga Mpina ametembelea maonesho ya wakulima nanenane kanda ya mashiriki inayoundwa na Mikoa Nne ya Pwaani,Tanga Morogoro na Dar es salaam na kuonesha kulidhishwa na kazi kubwa zinazofanywa na waandaaji wa maeonesho hayo.

Akizungumza mara baada ya kujionea kazi zinazofanywa katika maonesho hayo Waziri Mpina amesema Mwaka huu washiriki wametumia ubunifu mkubwa ambao utaleta tija katika uzarishaji kwa wakulima,wavivi na wafugaji watakaotembelea maonesho hayo.

Aidha amezitaka Taasisi na Mashirika yanayoshiriki katika maonesho ya wakulima nanenane kuwa na takwimu pamoja na taarifa zote sahihi zinazohusika katika mabanda yao bila ya kuweka mipaka ya kikanda ili kuweza kujibu hoja zinazoibuliwa na wadau wanaotembelea maonesho hayo.

Akiwa katika banda la wakala wa huduma za misitu Tanzania TFS waziri mpina ameitaka TFS kushikisha wananchi wakati wa kuweka mipaka ili kupunguza Migogoro ya Ardhi,huku Afisa habari wa TFS kanda ya mashariki Suleimani Burenda akisema wamejipanga katika kuzarisha asali na kulinda misitu iliyopo isihalibiwe na wanchi.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...