Search This Blog
Sunday, August 2, 2020
Rais wa Ufilipino: Sitanii - osheni barakoa kwa petroli'
Rais wa Ufilipino Rodrigo Duterte amesema kwa mara nyingine tena kuwa watu watumie petroli kuosha barakoa - na kusisitiza kwamba hafanyi mzaha.
Alisema maneno kama hayo wiki iliyopita lakini maafisa walimrekebisha haraka sana na akasema kwamba huo ulikuwa mzaha.
Maafisa wa afya wanasema kuwa barakoa zilizotengenezwa kwa kitambaa cha nguo zinatakiwa kuoshwa kama kawaida na zile barakoa zingine zitumike mara moja tu na kutupwa.
Lakini Ijumaa, rais huyo alisisitizia matamshi yake na kuongeza "kile nilichosema ni ukweli… nendeni kwenye kituo cha petroli".
Hakuna ushahidi wowote kwamba petroli inaweza kutumiwa kuua vijidudu kwenye barakoa; na kuitumia kwa muda mrefu kunaweza kusababisha hatari na kuinyunyizia vioevu kunaweza kusababisha moto.
Akirejelea matamshi yake ya awali, Bwana Duterte alisema: "Wakosoaji wanasema, 'Duterte ana kichaa.' Ni mpumbavu! Ikiwa mimi ni mpumbavu, wewe unastahili kuwa rahisi, sio mimi.
"Kile nilichosema ni cha kweli. Ikiwa pombe haipatikani, hasa kwa maskini, nenda tu kwenye kituo cha petroli, na utumie petroli kuua vijidudu.
"Sio utani. Sio mzaha. Wewe… wewe jitahidi kuwa na mawazo kama yangu."
Alisema nini wiki iliyopita
Bwana Duterte alisema wale ambao hawana vifaa vya kusafisha wanaweza kutumia petroli kusafisha barakoa zao.
"Mwisho wa siku, tundika [barakoa] sehemu na uinyunyize dawa ya kuzuia na kuua bakteria ya Lysol kama una uwezo," alisema, akirejelea dawa maarufu ya kuua vijidudu.
"Kwa watu wasio na [Lysol], itumbukize kwenye petroli au diseli... tafuta petroli kidogo na utumbukize mikono yako ikiwa imeshika barakoa."
Baada ya matamshi ya wiki iliyopita, msemaji wa serikali Harry Roque mara moja alimrekebisha.
"Siwezi kuamini kwamba baada ya miaka minne ya urais, bado hujui [yeye]," amesema Bwana Roque, kwa mujibu wa tovuti ya habari ya Rappler.
"[Ni utani] tu. Kwanini tutumie petroli kuosha kitu?"
Wakati huohuo afisa wa afya Maria Rosario Vergeire amesema barakoa za nguo zinastahili kuoshwa na kukaushwa kama kawaida, na zile zingine zitumiwe mara moja na kutupwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Punguza kilo tano kwa siku saba
NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...
-
Kiwanja kinauzwa kipo Dodoma Mahungu njia ya kwenda Singida kabala hujafika NALA. Kiwanja ni cha Makazi kinaukubwa wa Sqm 450 ( 15 X...
-
Akionekana kwa mara ya kwanza kwa umma tangu aondoke madarakani, aliyekuwa Rais wa Marekani Donald Trump ameweka wazi uwezekano wa kuwania...

No comments:
Post a Comment