Search This Blog

Wednesday, August 26, 2020

Takukuru kukagua Miradi ya Maendeleo Manyara



Na John Walter-Manyara 

Ili kudhibiti ubadhirifu wa fedha za Umma zinazotolewa kufanya miradi ya Maendeleo maeneo mbambali ya mkoa wa Manyara,Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa (TAKUKURU) Mkoa wa hapo, imeanza kutembelea na kukagua  miradi inayoendelea kwa sasa mkoani humo.

Afisa wa TAKUKURU wilayani Kiteto kitengo cha udhibiti na ufuatiliaji wa miradi ya Maendeleo Emmanuel Manyutwa,  amefika katika shule ya Msingi Partimbo  kukagua maendeleo ya ujenzi wa choo chenye matundu (20) kujiridhisha na fedha iliyotumika ukilinganisha na kazi iliyofanyika.

Hata hivyo Manyutwa ameridhika kuhusu maendeleo ya mradi.

Kwa mujibu wa Mkuu wa  TAKUKURU Mkoa wa Manyara Holle Makungu, Mradi huo ni kati ya miradi inayotekelezwa wilayani kiteto kupitia mpango  wa SWASH (School Water,Sanitation and Hygen) ambao Thamani yake ni shilingi Milioni 21,756,000/ hadi kukamilika.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...