Search This Blog

Wednesday, August 26, 2020

Mshambuliaji wa Christchurch afungwa maisha jela





Mshambuaji wa kizungu ambaye aliwauwa kwa bunduki waumini 51 kwenye misikiti miwili nchini New Zealand amehukumiwa kifungo cha maisha jela na kwa sharti kwamba muda wa kifungo hicho hauwezi kupunguzwa.

Jaji Cameron Mander amesema hukumu hiyo ambayo ndiyo ya juu zaidi na kwanza ya kutolewa nchini New Zealand inalenga kuonesha jinsi matendo ya mshambuliaji huyo Brenton Tarrant yalivyokosa utu na ubinadamu.

Jaji Mander ameongeza kusema kuwa makosa yaliyofanywa na mwanaume huyo raia wa Australia ni ukatili wa kiwango kibaya ambao hata hukumu ya maisha jela haiwezi kufuta hasara na maumivu aliyosababisha.

Katika mashambulizi ya Machi 2019, Tarrant aliwashambulia kwa bunduki za rashasha waumini waliokuwa kwenye ibada katika msikiti wa Al Noor na Linwoood mjini Christchurch.

Tangu mwezi Machi mwaka huu Tarrant alikubali mashtaka yaliyokuwa yakimkabili. Mshambuliaji huyo alisema anakiri kuwa na hatia ya kuwauwa waumini 51, na jaribio la kuwauwa wengine 40 katika mashambulizi ya bunduki aliyoyafanya mwezi Machi mwaka 2019.

Kisa hicho kiliutikisa ulimwengu na jamii za watu wa New Zealand ambayo ilifanya mageuzi ya sheria zake na kupiga marufuku umiliki wa bunduki za kivita.

Mtandao wa facebook pia ulitangaza kuwa utatilia mkazo uwezo wa kupeperusha matangazo moja kwa moja baada ya Tarrant kutumia mtandao huo kupeperusha moja kwa moja mashambulizi yake dhidi ya misikiti miwili mjini Christchurch.

Baadaye Ardern na Macron watatoa wito huo wa Christchurch kukabiliana na kusambaa kwa habari za chuki na zinazohusiana na masuala ya kigaidi pamoja na viongozi kutoka Uingereza, Canada, Norway, Jordan na Senegal ambao pia watakuwa mjini Paris.

Mpango huo unanuia kutoa shinikizo kwa kampuni za mitandao ya kijamii ambazo zinakabiliwa na miito zaidi kutoka kwa wanasiasa kutoka kote ulimwenguni kuzuia mitandao yao kutumiwa vibaya.

Baada ya kutokea shambulizi hilo, mjini  Christchurch, New Zealand  na  duniani  kwa  jumla  kulikuwa   na  mikesha, sala, kumbukumbu  na  ujumbe wa  mshikamano.

Neuseeland Polizistinnen tragen schwarze Kopftücher (picture-alliance/AA/P. Adones)

"Tuko  pamoja na  ndugu  zetu  Waislamu," ni  maneno  katika  bango  kubwa  jekundu miongoni  mwa  maua mengi  yaliyowekwa  katika  sehemu  moja  katika  kile  wakaazi  waliochosema  kuwa  ni "mji wa  huzuni".

Katika "kanisa  kuu  la mbao"  mjini  Christchurch, lililojengwa  baada  ya   tetemeko  la  ardhi  la  mwaka 2011 ambalo bado  limeweka  doa  katika  mji  huo , Dean Lawrence Kimberley aliendesha  misa  katika  kuonesha "mshikamano na  jamii  ya  waislamu."

Mjini Auckland , wakaazi  wa  jamii  zote  waliokuwa wakitiririkwa  na  machozi  walisimama  wakishikana  mikono  nje  ya  msikiti  wa  Umar kutoa heshima  zao.

Katika  eneo  la  bahari  ya  Tasmin , Waaustralia  waliopatwa  na  mshituko kwamba  kitendo  kama  hicho  katika  taifa  hilo  ndugu kimefanywa  na  mmoja  wao, waliapa kutoa  msaada  wowote ule  wanaoweza.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...