Search This Blog

Monday, August 10, 2020

RC KUNENGE AFANYA ZIARA YA KUTATUA KERO ZA WANANCHI PUGU.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amefanya ziara ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi Pugu Stesheni ambapo ameahidi kuzipatia ufumbuzi kero mbalimbali zinazowakabili wananchi hao.

Katika ziara hiyo RC Kunenge amepokea changamoto mbalimbali ikiwemo za elimu, miundombinu, maji, umeme, afya, migogoro mbalimbali na changamoto za kisheria ambapo zipo alizotatua papo kwa papo na nyingine kuzipatia utatuzi kwa kuwaelekea watendaji kuhakikisha wanazishughulikia Mara moja.

Kwenye ziara hiyo RC Kunenge aliambatana na watendaji mbalimbali wa Mkoa akiwemo katibu tawala wa Mkoa, wakuu wa idara pamoja na viongozi wa Wilaya ya Ilala.










 


No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...