Search This Blog

Tuesday, August 11, 2020

Denmark na Tanzania zaimarisha ushirikiano katika sekta ya maji

 

Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amekutana na kuzungumza Balozi wa Denmark nchini Tanzania, Mhe. Mette Dissing Spandet kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo kwenye Sekta ya Maji.

Mazungumzo hayo ya awali yalilenga ufadhili wa utekelezaji wa ujenzi wa miradi ya maji hususan kwenye maeneo ya usambazaji wa majisafi na usafi wa mazingira kwenye  majiji ya Dodoma na Dar es Salaam, kabla ya kukutana tena na kujadili masuala ya kiufundi katika kutekeleza miradi hiyo.

Kikao hicho kilihusisha wajumbe kutoka Wizara ya Maji, Mkuu wa Masuala ya Ushirikiano katika Ubalozi wa Denmark, Mette Bech pamoja na Msimamizi wa Idara ya Uwekezaji na Biashara katika Ubalozi wa Denmark, Oscar Mkude.



No comments:

Post a Comment

Punguza kilo tano kwa siku saba

  NI watu wachache wanaopenda kunenepa, wengi wanapenda miili ya wastani kwa kuwa  unene si mzuri. Ukiwa mnene si tu kwamba unakaribisha m...